Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya CNN ya Marekani imenukuu matokeo ya utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Monmouth yanayoonesha kuwa, asilimia 73 ya Wamarekani waliohojiwa wanaitakidi kuwa nchi yao inaelekea kusiko.
Ripoti hiyo imeeleza bayana kuwa, robo tatu ya watu waliohojiwa kwenye utafiti huo walitumia maneno hasi kuhusu hali ya hivi sasa ya Marekani.
Watafiti wa uchunguzi huo wa maoni waliwataka waliohojiwa kuieleza Marekani kwa neno moja, na neno lililotumika zaidi ni 'mgawanyiko' na maneno yanayoshabihiana na neno hilo kama mpasuko, mparaganyiko na mzozano.
342/